
Maandamano nchini Nigeria kutaka wasichana waliotekwa nyara kuachiliwa
Jeshi la Nigeria lilipata onyo la mapema kuhusu utekaji nyara wa wasichana 270, lakini likakosa kuchukua hatua zozote.
Taarifa hii ni ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.Wasichana 53 waliweza kutoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram na kuwaacha wasichana wengine 200 wakiwa mateka.
Maafisa wa serikali bado hawajatoa tamko lolote kuhusu madai ya Amnesty. Wakati huohuo Boko Haram wamesema kuwa watawauza wasichana hao.

Mzazi wa mmoja wa wasichana waliotekwa nyara
Kadhalika shirikla la Amnesty linasema licha ya onyo kutoka kwa Boko Haram , jeshi halikuchua hatua zozote kuzuia tukio hilo la utekaji nayar aktika kijiji cha Chibok.
Shirika hilo linasema kuwa kulikuwa na wasiwasi wa jeshi kupigana na kundi la Boko Haram ambalo linaonekana kuwa na zana nzito kuliko jeshi.
Inaaminika kuwa wasichana hao wamezuiliwa katika msitu mkubwa kutoka Chibok ambako wasichana wlaitekwa nyara hadi katika eneo la mpaka na Cameroon.
Boko Haram wamekiri kuwateka nyara wasichana hao wakisma kuwa hawapaswi kuwa shuleni wakisoma bali wanapaswa kuolewa na kuwa wake wa watu.
Kundi hilo limekuwa likipinga elimu ya kimagharibi tangu kuanza harakati zake katika jimbo la Borno mwaka 2009.
Takriban watu 1,200 wanaaminika kuuawa katika ghasia zilizosababishwa na kundi hilo mwaka huu pekee.
- Bbc
إرسال تعليق