Kanye West na Kim Kardashian wafunga ndoa ya kwanza kimya kimya Marekani

Kwa mujibu wa jarida la Life & Style Weekly, rapper Kanye West na Kim Kardashian sasa ni mume na mke halali baada ya kufunga ndoa kimya kimya huko California, Marekani wiki iliyopita.
kimye
Kwa mujibu wa chanzo, couple hiyo imekuwa wanandoa halali baada ya kupata leseni ya ndoa.
“Kim and Kanye are now married on paper. They got their license in California over the past few days,” Kilisema chanzo hicho.
Siku chache zilizopita Radar Online iliripoti kuwa couple hiyo italazimika kufunga ndoa mara tatu, ya kwanza ikiwa ni ya kiserikali ambayo ndio wamefunga wiki iliyopita nchini Marekani, ambayo sasa itafuatiwa na zingine mbili huko Ufaransa.
Chanzo kiliongeza kuwa sheria za Ufaransa zinahitaji wanandoa kufunga ndoa ya kiserikali nchini humo kabla ya ile ya kanisani, hivyo kwa Kim na Kanye watakuwa wamefunga ndoa mara tatu pamoja na waliyofunga Marekani.
Couple hiyo inatarajiwa kufanya sherehe rasmi ya ndoa jijini Paris, Ufaransa May 24 itakayoshuhudiwa na ndugu na marafiki wasiopungua 200 watakaoalikwa.

Post a Comment

أحدث أقدم