Keisha afunguka kuhusu Kujifungu Haraka haraka mtoto wa pili na Jina lake - Soma/Msikilize Hapa


MSANII wa Bongo Fleva,Khadija Shaban’ keisha’ wiki iliyopita alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Mkombozi Moroco, Jijini Dar es salaam, na huyo ni mtoto wa pili kwa Keisha na mume wake anayeitwa Jamal, mtoto wao wa kwanza walimwita Jam Kei (yani Jam ni Jamal jina la dingi na Kei ni Keisha jina la mama.Sasa Keisha amefunguka sababu ya kujifungu fasta fasta ingawa vigezo na masharti ya uzazi wa mpango vimezingatiwa kwani watoto hao wamepishana miaka mitatu.Aidha keisha amefunguka sababu ya kuzaa hivyo ni kwasababu amezaliwa peke yake, ameamua kuiongeza familia yao, lakini amesema sasa hivi atapumzika hata miaka saba bila kubeba ujauzito.

Post a Comment

Previous Post Next Post