MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MWANZA, ZANZIBAR ANGALIA PICHA HAPA
Hisia0
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa
heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo
yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiingia uwanjani CCM Kirumba
Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza .
Wafanyakazi wa Idara ya Maliasili wakiingia uwanjani CCM Kirumba katika kuhitimisha siku ya wafanyakazi..
Mahakama ya Tanzania wakiingia uwanja wa CCM Kirumba huku wakitanguliza ujumbe mzito.
Kibanda cha Veta kilikuwa moja ya vibanda vilivyovutia kwenye
maonyesho ya Siku ya Wafanyakazi zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba mkoani Mwanza.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakielekea kuingia kwenye
matembezi ya mshikamano katika kusheherekea siku ya Wafanyakazi kwenye
Viwanja vya CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakipita ya mgeni wa
heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo
yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein kushoto anaepunga mkono akiyapokea
maandamano ya Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku
ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini
Zanzibar.
Mashirika
mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni Rasmi hayupo pichani katika
Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli
ya Bwawani Mjini Zanzibar.Baadhi
ya Mawaziri pamoja na Wananchi waliohudhuria katika Maadhimishi ya siku
ya Wafanyakazi Duniani(May Day)wakiwa ndani ya Ukumbi wa Salama Holl
Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein watatu kulia akishikana mikono pamoja na
Viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Mshikamano kwa wafanyakazi ndani
ya Ukumbi wa Salama Holl Bwawani Hotel mjini Zanzibar ikiwa ni
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day).
إرسال تعليق