Serikali
inatarajia kununua magari mapya 700 kwa ajili ya polisi ambayo yatatumika
katika shughuli mbalimbali ikiwemo Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
Hatua
hiyo inatokana na Serikali kujipanga kudhibiti uhalifu kwa kuhakikisha polisi
wanakuwa na vifaa vya kisasa vitakavyowasaidia kupambana na uhalifu.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati
akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo cha kujadili bajeti
iliyopita ya mwaka 2013/2014 na inayokuja ya 2014/2015.
Alisema
kuwa Wizara yake inatarajia kutumia Sh bilioni 955.9 ambazo kati ya hizo Sh
bilioni 691.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 264.3 zikiwa ni
za maendeleo.
"Idara
ya Polisi ina uwezo wa kukusanya fedha nyingi na kwa mwaka huu imekusanya zaidi
ya asilimia 120 kwa miezi mitatu tu," alisema Waziri Chikawe.
Alisema
magari hayo yatakuwa kwa ajili ya matumizi ya polisi kwa shughuli zao zote
ikiwemo kupambana na biashara haramu za dawa za kulevya, uchaguzi pamoja na
operesheni nyingine watakazokuwa wakifanya kwa ajili ya kuleta hali ya usalama.
Post a Comment