Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni marufuku kwa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya shughuli zake ndani ya Bunge la
Bajeti.
Alisema
hayo juzi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe
kutangaza baraza kivuli la mawaziri na kusema hicho ndiko kikosi cha ukawa
ndani ya Bunge.
Spika
Makinda alimtaka Mbowe kuhakikisha Ukawa inafanya kazi zake nje ya Bunge na si
ndani ya Bunge kwani wanapokuwa ndani ya Bunge wanakuwa ni kambi ya upinzani
bungeni na si vinginevyo.
“Ukawa
ndani ya Bunge haipo, mnakumbuka shuka kumekucha, baraza lenu ni International
Standard na miaka ya nyuma nilishawahi kuwashauri kitu kama hicho lakini
mkakidharau na kuona hakina maana, nawapongeza sana, lakini mmekumbuka shuka
kumekucha,” alisema.
Pia
Spika Makinda alilitaka baraza hilo kivuli kutoa ushirikiano na wabunge wengine
ili kufanya kazi ya kuendeleza watu.
“Watanzania
hawajui nani anatoka wapi ila wanachotaka ni maendeleo yatakayosaidia kuboresha
hali zao za maisha, wanataka kuona barabara nzuri na hata mazao yao
yananunuliwa,” alisema.
Uteuzi
huo ulihusisha vyama vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi ambapo baraza hilo
kivuli lina mawaziri 29 ambapo watashika nafasi za uongozi katika kipindi
kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Post a Comment