Na Miza Kona - Maelezo Zanzibar .
MAKAMO
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd amewataka viongozI kuacha
uchochezi wa migogoro ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji kwa
lengo la kujipatia manufaa yao .
Wito
huo ameutoa huko Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati alipokuwa
akifanya majumuisho ya majadiliano ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa
Fedha 2014/2015.
amesema
kuna baadhi ya viongozi wanawachochea wananchi kufanya migogoro kwa
sababu za kisiasa kitendo ambacho kinapelekea kukosa maendeleo ya nchi.
“Tuache
kuchochea wananchi kufanya migogoro,pia tuache kuchochea wananchi na
wawekezaji kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi ili serikali ipate pato
na wananchi wapate ajira na kukuza uchumi”, alifahamisha Balozi Seif.
Balozi
Seif amewasisitiza viongozi kuwashajihisha wananchi kuleta maendeleo na
kuepuka Uchochezi wa kisiasa kwa lengo la kukuza uchumi ili jamii iweze
kuhamasika na kudumisha amani.
Aidha
Makamo wa Pili wa Rais amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa
kutaja Majina ya viongozi wanapokuwa katika majukwaa ya kisiasa badala
yake wanadi sera za vyama vyao.
Amesema
viongozi wanapokuwa katika majukwaa ya siasa wanatakiwa kuwaelimisha
wananchi mambo ya maendeleo ya nchi na sio kujadili kwa kuwataja majina
watu kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha amani na utulivu uliopo.
“Ili
amani na utulivu iendelee nchini basi ni lazima wanasiasa kuachana na
tabia ya kujadili na kutajana majina ya watu katika majukwaa ya siasa,
mnatakiwa kukaa kwenye majukwaa kunadi sera za vyama na kuwaelimisha
wananchi jinsi ya kuleta maendeleo ya nchi”, alisisitiza Balozi Seif.
Aidha
Makamo huyo amefahamisha kuwa fedha za serikali zinatumika ipaswavyo
kama zilivyopangwa kinyume na baadhi ya watu wanavyodai kuwa zinatumika
kinyume na mahitaji yaliyopangwa.
Mapema
akifanya majumuisho hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mohammed Aboud Mohammed amewataka wajumbe hao kushirikiana kwa pamoja
na kuachana na malumbano ili kuweza kuimarisha uchumi wa nchi.
Aidha
amefahamisha kuwa ni vyema kuimarisha Muungano na kujadili mambo ya
msingi kwa kuondoa kero zilizopo kwa kujenga hoja zitakazopelekea
kupatikana Katiba bora.
Wajumbe
hao wameipitisha vifungu vya bajeti ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
kwa mwaka fedha 2014/2015 kwa kuidhinisha jumla ya Shl. 19,988,300,000.
إرسال تعليق