Na Othman Khamis Ame,
Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Zanzibar
inafikiria kujenga Ukumbi Mkubwa wa Heshima ili ipate fursa zaidi ya
kujitangaza katika Nyanja za Kimataifa Kiutalii.
Alisema
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zimebarikiwa kuwa na mandhari nzuri
sambamba na Rasilmali nyingi za kuvutia zinazoweza kutoa fursa kadhaa za
kuongezeka kwa uchumi.
Balozi
Seif alieleza hayo wakati akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Majaji
Wanawake Tanzania { TAWJA } ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Jaji
Engera Kileo hapo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Spring Mjini
Arusha.
Mazungumzo hayo yalifanyika mwishoni mwa Mkutano wa 12 wa Chama cha
Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } uliochukuwa siku Nne na kufanyika ndani
ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha {AICC }.
Alisema
Dunia inaelewa uzuri wa Tanzania Kiutalii na kimazingira jambo ambalo
Serikali kwa kushirikiana na taasisi na jumuiya za kiraia zinapaswa
kujiandaa mapema katika kujenga miundo mbinu itakayosaidia kuzitumia
vizuri rasilmali hizo pamoja na mandhari zilizomo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alivipongeza Vyama vya Majaji Wanawake vya
Dunia na Tanzania kwa uamuzi wao wa kuufanya Mkutano wa 12 wa Chama cha
Majaji Wanawake Duniani { IAWJ} kufanyika Nchini Tanzania.
Balozi
Seif alisema Mkutano huo kwa kiasi kikubwa umesaidia kuongeza Uchumi
na mapato ya Taifa kwa vile washiriki wa Mkutano huo wametumia fursa
kubwa ya kutembelea maeneo ya historia pamoja na mbuga za Taifa.
Mapema
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania {TAWJA } Jaji Engera
Kileo alisema Mkutano huo umeisaidia Tanzania kujitangaza vyema
kiutalii, kiutamaduni na kimazingira.
Jaji Engera alisema wajumbe wa Mataifa 50 kati ya 100 wanachama wa Chama
cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } yaliyojumuisha washiriki wapatao
550 katika Mkutano huo wamevutiwa na hali ya mazingira ya Historia ya
Tanzania.
Mwenyekiti
huyo wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania alieleza kwamba vikao vya
Chama cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } kimekuwa kikiendesha mikutano
yake kila baada ya miaka miwili katika nchi mbali mbali wanachama.
Alisema
Mkutano wa kwanza wa Chama hicho ulifanyika Nchini Argentina na huu wa
Tanzania ni mara ya pili kufanyika Barani Afrika
ukitanguliwa na ule wa Uganda mwaka 2008.
Wajumbe
wa Mkutano huo wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani walipata
fursa ya kujumuika pamoja katika chakula cha usiku kilichondaliwa maalum
kwa ajili ya kuagana baada ya kumaliza mkutano wao.
Tafrija
hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Maunt Meru ambapo mgeni rasmi alikuwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana
pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu.
Chakula
hicho cha usiku kiliambatana na ngoma za Utamaduni kutoka Kikundi cha
Jeshi la Kujenga Taifa { JKT } Kambi ya Oljoro pamoja na Muziki wa
waimbaji mbali mbali ndani na nje ya Nchi ambapo Wajumbe hao walipata
fursa ya kujimwaga vyema uwanjani.

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkewe Mama
Pili Juma Iddi kulia wakiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande
Othman kwenye tafrija maalum kwenye Hoteli ya Mount Meru baada ya
kumalizika kwa Mkutano wa Chama cha Majaji Wanawake uliofanyika Mkoani
Arusha.

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake wa Philippines Jaji Teresita
Leonardo – De Castro. Kushoto Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed
Chande Othman.

Kikundi
cha Utamaduni cha Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro kikitumbuiza ngoma
maarufu ya Kibati yenye Asili ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye Tafrija
ya Chama cha Majaji Wanawake Duniani iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount
Meru Arusha.

Baadhi
ya Wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani
wakijipatia chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa Mkutano wao wa
siku Nne Mjini Arusha.

Baadhi
ya Wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani
wakijipatia chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa Mkutano wao wa
siku Nne Mjini Arusha.

Mwenyekiti
wa Chama cha Majaji Wanawake kutoka Nchini Philippines Jaji Teresita
Leonardo – De Castro akifurahia chakula murua cha kitanzania
kilichoandaliwa kwa wajumbe wa Mkutano wa Chama cha Majaji Wanawake
Duniani Mjini Arusha Tanzania

Mwenyekiti
wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } Jaji Eusebia Munuo
akijipatia mlo kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya
Wajumbe wa Mkutano huo wa 12.

Jaji
Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akijumuika pamoja na wajumbe
wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani kwenye chakula cha usiku
kilichoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao.Kulia
ya Jaji Chande ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu
akipatiwa huduma za mlo na Mkuu wa Mapishi wa Hoteli ya Mount Meru
Prosper Makongo.

Bendi
ya Kibo Sounds ikiendelea kutumbuiza kwenye tafrija ya chakula cha
usiku kwa ajili ya wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake
Duniani hapo Mount Meru Hoteli Arusha.

Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa Jaji Sanji Mmasenono
Monageng Raia wa Jamuhuri ya Botswana akifurahia Tuzo Maalum
aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani Jaji
Eusebia Munuo kushoto yake kwenye Tafrija ya Wajumbe wa Mkutano huo
iliyofanyika Mkoani Arusha.Pembeni
yao kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani
{ IAWJ } anayefanya kazi zake Makuu ya Chama hicho Mjini Washington
Marekani Jaji J. Winship.

Jaji
Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akitoa neno la shukrani
kwenye tafrija maalum ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili ya
Wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani hapo
Hoteli ya Mount Meru Arusha.

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na
Mjumbe wa Chama cha Majaji Duniani kutoka Nchini Swatzeland Jaji
Sandry kwenye Tarija maalum ya Wajumbe wa Mkutano wa Majaji Wanawake
Duniani.

Wajumbe
wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani wakiserebuka
kwenye Ngoma za hali ya juu zilizochaguliwa maalum kuwaburudisha baada
ya kumaliza kazi ngumu ya Mkutano wao uliofanyika Mjini Arusha.

Wajumbe
wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani wakiserebuka
kwenye Ngoma za hali ya juu zilizochaguliwa maalum kuwaburudisha baada
ya kumaliza kazi ngumu ya Mkutano wao uliofanyika Mjini Arusha.

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati
akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake cha
Tanzania { TAWJA } Engera Kileo alipofika kwa mafungumzo hapo Hoteli ya
Naura Spring iliyopo Arusha. Kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Jaji Imani Aboud.

Mwenyekiti
wa Chama cha Majaji Wanawake cha Tanzania { TAWJA } Engera Kileo
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye
Hoteli ya Kimataifa ya Naura Spring Mjini Arusha. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Post a Comment