Maulamaa wa Somalia washika silaha kupambana na itikadi ya al-Shabaab

Na Bosire Boniface, Garissa

Shekhe Abass Mohamud siyo tu imamu ambaye hasa hutoa muhadhara katika misikiti na kuongoza waswaliji.

Pia huchukua silaha na kupambana na al-Shabaab pamoja na vikosi vya Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) .

Mohamud, mwenye umri wa miaka 55, imamu wa msikiti katika mji wa Ras Kamboni katika mkoa wa Jubba ya chini, alisema alishuhudia vikundi mbalimbali vikizuia jitihada za kujenga Somali yenye amani na imara. Lakini hadi sasa, alisema, al-Shabaab ni kitisho kikubwa cha utawala wa sheria ambacho nchi inakabiliana nacho.

"Al-Shabaab ni tofauti na vikundi vingine kwa sababu kinatumia itkadi [ya dini] iliyopotoshwa kuhalalisha vurugu zisizochagua kwa uangalifu Waislamu na watu wengine wasio na hatia," aliiambia Sabahi.

Mohamud alisema aliamua kujiunga na vikosi shirika ili kurejesha amani nchini Somalia na kukabili itikadi ya uongo ya al-Shabaab.

Itikadi iliyopotoshwa ya Al-Shabaab

Mzee wa Kisomali akiwa amesimama karibu na mwombaji wake wakati wa maandamano ya wanamgambo wa ndani, iliyoundwa ili kutoa usalama wa mji wa Marka tarehe 30 Aprili. Maulamaa na Mashehe wa Somalia pia wamejiunga na jitihada hizo za vita kuwatokomeza al-Shabaab. [AU UN IST PHOTO / Tobin Jones]

" itikadi iliyopotoshwa kwamba al-Shabaab inaeneza Uislamu unaogopesha, imani ya Kiislamu, na imeweka dini ya amani ya Kiislamu kwenye njia panda na imani nyingine," alisema. "Ni lazima nioanishe kuwaongoza waswali na kufanya mahubiri kuhusu kanuni za kweli za Kiislamu pamoja na kupambana na hao yanaopotosha [dini hii] kupata matakwa [yao binafsi]."

" itikadi iliyopotoshwa kwamba al-Shabaab inaeneza Uislamu unaogopesha, imani ya Kiislamu, na imeweka dini ya amani ya Kiislamu kwenye njia panda na imani nyingine," alisema. "Ni lazima nioanishe kuwaongoza waswali na kufanya mahubiri kuhusu kanuni za kweli za Kiislamu pamoja na kupambana na hao yanaopotosha [dini hii] kupata matakwa [yao binafsi]."

Mohamud alisema anajua atakuwa mlengwa wa al-Shabaab kwa "kuungana na" hao wanaoitwa wasioamini, lakini hataruhusu hilo kuzuia jitihada zake.

"Kifo ni majaliwa ya Mungu [kwetu sisi]. Kila mmoja nchini Somalia ni mlengwa wa kikundi hicho. Kama iliandikwa kwamba nitakufa katika uwanja wa mapambano, siwezi kuzuia hilo," alisema. "Lakini ninataka kulinda mafundisho sahihi ya Kiislamu na watu."

Mohamud alisema kusudi lake la kupambana na al-Shabaab lilimupeleka mbali na wilaya yake ya nyumbani ya Badhaadhe.

"Kundi hilo bado linadhibiti baadhi ya maeneo ya Somalia na kwa kuwa niko mzima na nina afya njema, nitashirikiana na jeshi la Somalia na vikosi vilivyofungamana nalo katika uwanja wa mapambano," alisema, akiongeza kwamba alifundishwa na kufanya kazi katika jeshi kwa miaka minne kabla halijavunjwa mwaka 1991.

Alisema ushiriki wake katika vita ulikuwa zaidi ya mfano, kwa kuwa ana uelewa kuhusu ardhi na alama za ardhini katika eneo la kusini mwa mkoa ambako vikosi vilivyofungamana vinapamabana na wanamgambo.

Mohamud, ambaye alishika silaha mara baada Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kuingia Somalia mwaka 2011, sio kiongozi wa dini tu aliyeshirikishwa katika mapigano.

"Maulamaa katika SNA walishiriki katika kuzungumza na umma kuhusu kukubali SNA na vikosi vya AMISOM kufungamana katika vita dhidi ya al-Shabaab," alisema, akiongeza kwamba kwa sababu mashehe wanasikilizwa sana katika jamii, walitumika kupata taarifa kuhusu maeneo waliyojificha al-Shabaab, shughuli na mipango yao.

Kupambana na al-Shabaab ni wajibu wa kidini
Shehe anayeishi Dobley Hassan Salat, mwenye umri wa miaka 45, alisema anaamini kwamba mapambano ya al-Shabaab na jeshi la Somalia ni wajibu wa kidini anaopaswa kuufanya.

"Wanachama wa al-Shabaab hawatasita kuwaua watu wasiokuwa na hatia," aliiambia Sabahi. "Hivyo, katika kujilinda na kutetea umma kwa ujumla, mimi ni sehemu ya jeshi la Somalia ambalo linaendesha uvamizi wa maficho ya maeneo ya kundi hilo, kuwaua au kuwateka wakiwa katika mchakato."

Salat alisema alijiunga na mapigano katika uwanja wa mapambano ili vizazi vijavyo vya Somalia hatimaye viweze kufurahia amani na utulivu ambao ulikosekana nchini kwa zaidi ya miaka 20.

"Ninapochukua silaha yangu ya moto kupamabana na al-Shabaab, nilikuwa pia ninapeleka ujumbe kwa umma kwa ujumla kwamba kundi hilo linakosea," alisema. "Ni muhimu kwamba tuungane kupamabana na watu ambao wanawaua watu wasiokuwa na hatia [kwa msingi] wa itikadi zilizobadilishwa."

Kama Mohamud, Salat pia alisema alipata vitisho kutoka kwa al-Shabaab lakini hatatuliza vita dhidi ya wenye itikadi kali.

"Ninajua wao ni hatari sana na kwamba wamefanya majaribio mengi katika maisha yangu, lakini nipo tayari kujitolea kila nilichonacho, hata maisha yangu, kwa faida ya raia ambao wamepata shida kwa miaka yote hii," alisema.

"Kundi hili limewaua maulamaa wengi sana ambao walizungumza dhidi ya shughuli zao haramu lakini sina wasiwasi," alisema.

Salat alisema aliandaa mkutano wa umma katika makazi ya mjini na pia wakati akiwa katika misheni na vikosi washirika ili kuwasiliana na raia na kuwashawishi kupingana na msimamo mkali.

"Ninatumia fursa ya mkusanyiko kuhubiri kupingana na al-Shabaab wakati pia [ninafundisha] dini ya Kiislamu kwa ujumla," alisema.

Balozi wa Somalia nchini Kenya Mohammed Ali Nur alisema wahubiri wengi wa Kiislamu walikuwa wanapigana pamoja na SNA na vikosi washirika ili kuwaondoa al-Qaeda-washirika wa wanamgambo wa al-Shabaab. "Kama vile ilivyo kwa Wasomali wengine, maimamu na mashehe wanahamasishwa na hamu ya kuwa na amani na utulivu, sio katika Somalia tu bali katika kanda na duniani," Nur aliiambia Sabahi.

"Ni jukumu la Wasomali kuungana -- ama kwa kupigana ana kwa ana na kikundi, kujitolea kutoa taarifa kwa serikali ya Somalia ambayo inaweza kusaidia kulitokomeza kundi au kuondoa itikadi za kupotosha za kikundi," alisema.

Kuimarisha imani ya wanajeshi, kunakaza kitanzi kwa al-Shabaab
Zaidi ya mashehe na wahubiri wa Somalia kuchangia katika jitihada za vita, KDF ina wahubiri wake wanaopigana katika vita, kwa mujibu wa msemaji wa KDF Kanali Willy Wesonga.

KDF ina wahubiri wa Kikristo na Kiislamu katika uwanja wa vita ambao wanatoa ushauri wa kiroho na kihisia kwa wanajeshi wenzao, aliiambia Sabahi. Wahubiri pia ni watumishi wenye fani ya jeshi ambao wana silaha za kupambana na adui, alisema.

"Wanajeshi wako katika mstari wa mbele vitani wakihatarisha maisha yao kwa maslahi bora ya Somalia, Kenya na kanda," alisema. "Kama wanajeshi wengine, [wahubiri] wamejitoa mstari wa mbele vitani ili kukomesha shughuli za kikundi cha ugaidi."

Kapteni wa KDF Mohammed Dek Sahid, ambaye pia anafanya kazi ya uimamu katika msikiti wa kambi ya jeshi nchini Kenya, alisema wahubiri katika uwanja wa vita walijitolea kuilinda Somalia na Kenya.

"Tunayajali mataifa yote mawili," alisema Sahid, aliyekuwa kiongozi wa dini na kupata cheti katika masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Mbeere kabla ya kujiunga na jeshi. "Hatukazi kitanzi tu kwa al-Shabaab bali pia kuimarisha imani ya wanajeshi."

"Al-Shabaab wana bendera nyeusi na [inamaanisha] vurugu, lakini tuna kazi ya kuilinda bendera ya bluu ya Somalia na kufundisha dini ya kweli ya Kiislamu, ambayo inamaanisha amani," aliiambia Sabahi.

"Popote nafasi inapojitokeza ya kuzungumza na umma, tunawaeleza kwamba itikadi za msimamo mkali hazina nafasi katika Uislamu," alisema. "Hii sio kuhusu kupigana tu vita vya ana kwa ana bali pia vya kiroho. [Mafundisho] kanuni sahihi za Kiislamu ni muhimu sana katika kupinga mapambano ya itikadi dhidi ya al-Shabaab na kuteka mioyo na akili za raia."

Post a Comment

Previous Post Next Post