Na RFI
Mashirika ya kutetea haki za bunadamu likiwemo shirika la Amnesty
International juma hili yametoa wito kwa serikali ya mamlaka ya
Palestina kutia saini mkataba unaotambua mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita ya ICC.

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud
Abbas akiombwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu kutia sani ya
kuitambua mahakama ya kimataifa ICC..
Reuters/Mohamad Torokman
Mashirika zaidi ya kumi na saba ya ndani ya Palestina na yale ya
kimataifa likiwemo shirika la Amnesty International, kwa pamoja
wamemuandikia barau rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas kutia
saini mkataba wa Roma kujiunga na mahakama ya ICC.
Mashirika hayo kwenye maelezo yake, yamesema kuwa kujiunga kwa mamlaka
ya Palestina kwa kutia saini makataba wa Roma kutaifanya nchi hiyo
kupata haki hasa kwa viongozi wake ambao waliuawa ndani na nje ya
palestina.
Mratibu wa shirika la Amnesty kwenye ukanda wa mashariki ya kati na
Afrika Kaskazini, Philip Luther amesema kuwa mkataba huo utaiwezesha
mahakama ya ICC kuwafungulia mashtaka wahalifu wa kivita waliotenda
makosa ndani na nje ya mamlaka ya Palestina.
Mwezi April mwaka huu rais Abbas alitia saini mkataba wa kujiunga na
mashrika 15 ya umoja wa mataifa hatua iliyopelekea kuvunjika kwa
mazungumzo ya amani kati yake na Israel.
Nchi ya Israel na Marekani zimekuwa mstari wa mbele kuyashawsihi
mashirika ya Umoja wa mataifa kuitambua mamlaka ya Palestina mpaka pale
kutakapopatika suluhu kati yake na Israel.
Source: kiswahili.rfi.fr
Source: kiswahili.rfi.fr
Post a Comment