Na Bosire Boniface, Garissa
Shekhe Abass Mohamud siyo tu imamu ambaye hasa hutoa muhadhara katika misikiti na kuongoza waswaliji.
Pia huchukua silaha na kupambana na
al-Shabaab pamoja na vikosi vya Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) na
Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) .
Mohamud, mwenye umri wa miaka 55, imamu wa msikiti katika mji wa Ras
Kamboni katika mkoa wa Jubba ya chini, alisema alishuhudia vikundi
mbalimbali vikizuia jitihada za kujenga Somali yenye amani na imara.
Lakini hadi sasa, alisema, al-Shabaab ni kitisho kikubwa cha utawala wa
sheria ambacho nchi inakabiliana nacho.
"Al-Shabaab ni tofauti na vikundi vingine kwa sababu kinatumia itkadi
[ya dini] iliyopotoshwa kuhalalisha vurugu zisizochagua kwa uangalifu
Waislamu na watu wengine wasio na hatia," aliiambia Sabahi.
Mohamud alisema aliamua kujiunga na vikosi shirika ili kurejesha amani
nchini Somalia na kukabili itikadi ya uongo ya al-Shabaab.
Itikadi iliyopotoshwa ya Al-Shabaab

Mzee wa Kisomali akiwa amesimama karibu na
mwombaji wake wakati wa maandamano ya wanamgambo wa ndani, iliyoundwa
ili kutoa usalama wa mji wa Marka tarehe 30 Aprili. Maulamaa na Mashehe
wa Somalia pia wamejiunga na jitihada hizo za vita kuwatokomeza
al-Shabaab. [AU UN IST PHOTO / Tobin Jones]
" itikadi iliyopotoshwa kwamba al-Shabaab inaeneza Uislamu unaogopesha,
imani ya Kiislamu, na imeweka dini ya amani ya Kiislamu kwenye njia
panda na imani nyingine," alisema. "Ni lazima nioanishe kuwaongoza
waswali na kufanya mahubiri kuhusu kanuni za kweli za Kiislamu pamoja na
kupambana na hao yanaopotosha [dini hii] kupata matakwa [yao binafsi]."
" itikadi iliyopotoshwa kwamba al-Shabaab inaeneza Uislamu unaogopesha,
imani ya Kiislamu, na imeweka dini ya amani ya Kiislamu kwenye njia
panda na imani nyingine," alisema. "Ni lazima nioanishe kuwaongoza
waswali na kufanya mahubiri kuhusu kanuni za kweli za Kiislamu pamoja na
kupambana na hao yanaopotosha [dini hii] kupata matakwa [yao binafsi]."
Mohamud alisema anajua atakuwa mlengwa wa al-Shabaab kwa "kuungana na"
hao wanaoitwa wasioamini, lakini hataruhusu hilo kuzuia jitihada zake.
"Kifo ni majaliwa ya Mungu [kwetu sisi]. Kila mmoja nchini Somalia ni
mlengwa wa kikundi hicho. Kama iliandikwa kwamba nitakufa katika uwanja
wa mapambano, siwezi kuzuia hilo," alisema. "Lakini ninataka kulinda
mafundisho sahihi ya Kiislamu na watu."
Mohamud alisema kusudi lake la kupambana na al-Shabaab lilimupeleka mbali na wilaya yake ya nyumbani ya Badhaadhe.
"Kundi hilo bado linadhibiti baadhi ya maeneo ya Somalia na kwa kuwa
niko mzima na nina afya njema, nitashirikiana na jeshi la Somalia na
vikosi vilivyofungamana nalo katika uwanja wa mapambano," alisema,
akiongeza kwamba alifundishwa na kufanya kazi katika jeshi kwa miaka
minne kabla halijavunjwa mwaka 1991.
Alisema ushiriki wake katika vita ulikuwa zaidi ya mfano, kwa kuwa ana
uelewa kuhusu ardhi na alama za ardhini katika eneo la kusini mwa mkoa
ambako vikosi vilivyofungamana vinapamabana na wanamgambo.
Mohamud, ambaye alishika silaha mara baada Kikosi cha Ulinzi cha Kenya
(KDF) kuingia Somalia mwaka 2011, sio kiongozi wa dini tu
aliyeshirikishwa katika mapigano.
"Maulamaa katika SNA walishiriki katika kuzungumza na umma kuhusu
kukubali SNA na vikosi vya AMISOM kufungamana katika vita dhidi ya
al-Shabaab," alisema, akiongeza kwamba kwa sababu mashehe wanasikilizwa
sana katika jamii, walitumika kupata taarifa kuhusu maeneo waliyojificha
al-Shabaab, shughuli na mipango yao.
Kupambana na al-Shabaab ni wajibu wa kidini
Shehe anayeishi Dobley Hassan Salat, mwenye umri wa miaka 45, alisema
anaamini kwamba mapambano ya al-Shabaab na jeshi la Somalia ni wajibu wa
kidini anaopaswa kuufanya.
"Wanachama wa al-Shabaab hawatasita kuwaua watu wasiokuwa na hatia,"
aliiambia Sabahi. "Hivyo, katika kujilinda na kutetea umma kwa ujumla,
mimi ni sehemu ya jeshi la Somalia ambalo linaendesha uvamizi wa maficho
ya maeneo ya kundi hilo, kuwaua au kuwateka wakiwa katika mchakato."
Salat alisema alijiunga na mapigano katika uwanja wa mapambano ili
vizazi vijavyo vya Somalia hatimaye viweze kufurahia amani na utulivu
ambao ulikosekana nchini kwa zaidi ya miaka 20.
"Ninapochukua silaha yangu ya moto kupamabana na al-Shabaab, nilikuwa
pia ninapeleka ujumbe kwa umma kwa ujumla kwamba kundi hilo linakosea,"
alisema. "Ni muhimu kwamba tuungane kupamabana na watu ambao wanawaua
watu wasiokuwa na hatia [kwa msingi] wa itikadi zilizobadilishwa."
Kama Mohamud, Salat pia alisema alipata vitisho kutoka kwa al-Shabaab lakini hatatuliza vita dhidi ya wenye itikadi kali.
"Ninajua wao ni hatari sana na kwamba wamefanya majaribio mengi katika
maisha yangu, lakini nipo tayari kujitolea kila nilichonacho, hata
maisha yangu, kwa faida ya raia ambao wamepata shida kwa miaka yote
hii," alisema.
"Kundi hili limewaua maulamaa wengi sana ambao walizungumza dhidi ya shughuli zao haramu lakini sina wasiwasi," alisema.
Salat alisema aliandaa mkutano wa umma katika makazi ya mjini na pia
wakati akiwa katika misheni na vikosi washirika ili kuwasiliana na raia
na kuwashawishi kupingana na msimamo mkali.
"Ninatumia fursa ya mkusanyiko kuhubiri kupingana na al-Shabaab wakati pia [ninafundisha] dini ya Kiislamu kwa ujumla," alisema.
Balozi wa Somalia nchini Kenya Mohammed Ali Nur alisema wahubiri wengi
wa Kiislamu walikuwa wanapigana pamoja na SNA na vikosi washirika ili
kuwaondoa al-Qaeda-washirika wa wanamgambo wa al-Shabaab. "Kama vile
ilivyo kwa Wasomali wengine, maimamu na mashehe wanahamasishwa na hamu
ya kuwa na amani na utulivu, sio katika Somalia tu bali katika kanda na
duniani," Nur aliiambia Sabahi.
"Ni jukumu la Wasomali kuungana -- ama kwa kupigana ana kwa ana na
kikundi, kujitolea kutoa taarifa kwa serikali ya Somalia ambayo inaweza
kusaidia kulitokomeza kundi au kuondoa itikadi za kupotosha za kikundi,"
alisema.
Kuimarisha imani ya wanajeshi, kunakaza kitanzi kwa al-Shabaab
Zaidi ya mashehe na wahubiri wa Somalia kuchangia katika jitihada za
vita, KDF ina wahubiri wake wanaopigana katika vita, kwa mujibu wa
msemaji wa KDF Kanali Willy Wesonga.
KDF ina wahubiri wa Kikristo na Kiislamu katika uwanja wa vita ambao
wanatoa ushauri wa kiroho na kihisia kwa wanajeshi wenzao, aliiambia
Sabahi. Wahubiri pia ni watumishi wenye fani ya jeshi ambao wana silaha
za kupambana na adui, alisema.
"Wanajeshi wako katika mstari wa mbele vitani wakihatarisha maisha yao
kwa maslahi bora ya Somalia, Kenya na kanda," alisema. "Kama wanajeshi
wengine, [wahubiri] wamejitoa mstari wa mbele vitani ili kukomesha
shughuli za kikundi cha ugaidi."
Kapteni wa KDF Mohammed Dek Sahid, ambaye pia anafanya kazi ya uimamu
katika msikiti wa kambi ya jeshi nchini Kenya, alisema wahubiri katika
uwanja wa vita walijitolea kuilinda Somalia na Kenya.
"Tunayajali mataifa yote mawili," alisema Sahid, aliyekuwa kiongozi wa
dini na kupata cheti katika masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha
Mbeere kabla ya kujiunga na jeshi. "Hatukazi kitanzi tu kwa al-Shabaab
bali pia kuimarisha imani ya wanajeshi."
"Al-Shabaab wana bendera nyeusi na [inamaanisha] vurugu, lakini tuna
kazi ya kuilinda bendera ya bluu ya Somalia na kufundisha dini ya kweli
ya Kiislamu, ambayo inamaanisha amani," aliiambia Sabahi.
"Popote nafasi inapojitokeza ya kuzungumza na umma, tunawaeleza kwamba
itikadi za msimamo mkali hazina nafasi katika Uislamu," alisema. "Hii
sio kuhusu kupigana tu vita vya ana kwa ana bali pia vya kiroho.
[Mafundisho] kanuni sahihi za Kiislamu ni muhimu sana katika kupinga
mapambano ya itikadi dhidi ya al-Shabaab na kuteka mioyo na akili za
raia."
Chanzo: sabahionline.com

إرسال تعليق