
United wamekubaliana na Bayern Munich kuuziana Toni Kroos (katikati).
MANCHESTER United amekubaliana dili la kumsajili kiungo wa Bayern Munich,
Toni Kroos na sasa wanajipanga kuiwinda saidi ya mchezaji mwenzake, Mholanzi Arjen Robben.
Kross
alikubaliana na ofa ya paundi milioni 20 na aliyekuwa kocha wa
Manchester United, David Moyes na mrithi wake ambaye aliyewahi kuwa
kocha wa Bayern Munich, Louis Van Gaal amebariki dili hilo kuendelea.
Kroos,
24, aling`ara wakati wa utawala wa Van Gaal katika klabu ya Bayern na
bado anahitaji kufanya kazi na kocha wake wa zamani.
Yupo kwenye rada: United kwasasa wapo katika mawindo ya kumnasa nyota wa Bayern, Arjen Robben
Tabasamu tu: Kocha wa Uholanzi, Louis Van Gaal akitasamu katika mazoezi ya timu yake mjini Lagos nchini Ureno.
Robben ni
mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Van Gaal wakati akiwa Bayern kwa ada
ya uhamisho wa paundi milioni 20 kutokea klabu ya Real Madrid mwaka
2009.
Siku za
karibuni winga huyo mwenye miaka 20 alisaini mkataba wa miaka mitatu na
Bayern, lakini haimvunji moyo Van Gaal ambaye atafanya kazi na Robben
katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Inafahamika
kuwa United wamekubaliana dili la paundi milioni 27 ili kuinasa saini
ya beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw na beki wa kati wa
Borussia Dortmund, Mats Hummels yupo katika mipango ya Van Gaal.
إرسال تعليق