MANCHESTER CITY YATWAA KOMBE LA LIGI YA UINGEREZA 2013/14

 HATIMAYE timu Manchester City, imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu England kwa msimu wa 2013/14 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Wagonga Nyundo wa London, West Ham United katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester.
 Ushindi  huo, ulizima ndoto za miaka 24 kwa Majogoo wa Merseyside, Liverpool FC, ambao walikuwa wakiunyatia kwa karibu hadi dakika ya mwisho. Kiungo wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Samir Nasir ndiye alifungua karamu ya mabao dakika ya 39 kabla ya nahodha Vicent Kompany kufunga pazia la mabao kwa City msimu huu dakika ya 49.

 City, wamerekebisha makosa ya msimu ulioopita, baada ya kushuhudia Kombe likielekea mtaa wa pili; Manchester United, ambao msimu huu wamemaliza nafasi ya saba. Aidha kombe limebaki Jiji la Manchester kwa msimu wa nne mfululizo.
 Tukio la kipekee, mashabiki wab City walifurika uwanjani kuwazingira wachezaji wao kwa shangwe, jambo ambalo si kawaida Ulaya kutokana na sheria ya usalama wa wachezaji.
 Mashabiki wa Manchester City wakiingia uwanjani kushangilia ubingwa wa timu yao.
 Kwa upande mwingine  kichapo cha mabao 2-0 waliopokea Norwich City dhidi ya Arsenal, kimeishusha rasmi Norwich iliyoungana na Fulham na Cardiff City zilizotangulia mapema.
Wachezaji wa Man City wakishangilia bao lao la kwanza lililowekwa kimiani na Vicent Kompany. 
Bingwa mtetezi, Manchester United wao wamemaliza katika nafasi yao ile ile ya saba, licha ya kufunga pazia kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton ugenini.

Post a Comment

Previous Post Next Post