HATIMAYE
timu Manchester City, imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu
England kwa msimu wa 2013/14 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata
dhidi ya Wagonga Nyundo wa London, West Ham United katika mchezo
ulipigwa kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester.
Ushindi huo, ulizima ndoto za miaka 24 kwa Majogoo wa Merseyside,
Liverpool FC, ambao walikuwa wakiunyatia kwa karibu hadi dakika ya
mwisho. Kiungo wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Samir Nasir ndiye alifungua karamu
ya mabao dakika ya 39 kabla ya nahodha Vicent Kompany kufunga pazia la
mabao kwa City msimu huu dakika ya 49.
City, wamerekebisha makosa ya msimu ulioopita, baada ya kushuhudia Kombe
likielekea mtaa wa pili; Manchester United, ambao msimu huu wamemaliza
nafasi ya saba. Aidha kombe limebaki Jiji la Manchester kwa msimu wa nne
mfululizo.
Tukio la kipekee, mashabiki wab City walifurika uwanjani kuwazingira
wachezaji wao kwa shangwe, jambo ambalo si kawaida Ulaya kutokana na
sheria ya usalama wa wachezaji.
Mashabiki wa Manchester City wakiingia uwanjani kushangilia ubingwa wa timu yao.
Kwa upande mwingine kichapo cha mabao 2-0 waliopokea Norwich City dhidi
ya Arsenal, kimeishusha rasmi Norwich iliyoungana na Fulham na Cardiff
City zilizotangulia mapema.
Wachezaji wa Man City wakishangilia bao lao la kwanza lililowekwa kimiani na Vicent Kompany.
Bingwa
mtetezi, Manchester United wao wamemaliza katika nafasi yao ile ile ya
saba, licha ya kufunga pazia kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton
ugenini.
إرسال تعليق