Baada ya tuzo za KTMA kumalizika kila mmoja amekuwa na mtazamo
wake, wiki hii producer wa wimbo wa ‘Number One’ wa Diamond, Sheddy
Clever alitoa malalamiko yake ya kukosa tuzo ya mtayarishaji bora huku
wimbo alioutengeneza ukimpa Diamond zaidi ya tuzo tano.
Producer mkongwe Joachim Kimaryo aka Master J ametoa mtazamo wake
kuhusu tuzo za KTMA 2014 ambao unaonesha hakuridhishwa na mshindi wa
tuzo ya mtayarishaji bora wa mwaka – kizazi kipya ambaye ni Man Water
wa Combinenga.
“Sijaelewa damond kupata tuzo 7 alafu produza wake kutoka na 0!!!!!”
ni jibu la moja ya maswali kuhusiana na tuzo hizo aliyokutana nayo
Master J Jana alipokuwa mgeni katika session ya ‘Kikaangoni Live’
kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Shabiki mwingine aliuliza: “Pia man water ni mkali au unasemaje master J?”
Na hiki ndicho alichojibu Jay: “mkali lakini hakusahili kushinda mwaka huu”
Na hiki ndicho alichojibu Jay: “mkali lakini hakusahili kushinda mwaka huu”
Swali tofauti na muziki ambalo lilijirudia mara nyingi ni kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake Shaa, shabiki mmoja aliuliza:
“Mnafunga ndoa lini ww na Shaa manake mnapendezana kweli? Au ni mchepuko tu wa lami?
“Mnafunga ndoa lini ww na Shaa manake mnapendezana kweli? Au ni mchepuko tu wa lami?
Na jibu la Joachim aka Master J mabibi na mabwana lilikuwa “SOON”.
Post a Comment