MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI


 DSCF5413

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya makundi.
Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
“Ndugu tunashukuru kwa maombi yenu,  alichotupangia mungu ndicho tulichopata.  Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo basi tumeyaaga mashindano”. Amesema Freddy.

Post a Comment

Previous Post Next Post