Mgodi
wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama mkoani Shinyanga, huenda ukafungwa ndani ya
miaka miwili ijayo ili kuiepushia hasara kampuni inayochimba dhababu katika
eneo hilo, African Barrick Gold.
Meneja
mgodi huo, Muganda Mutereko alisema hali hiyo itatokea endapo bei ya dhahabu
itaendelea kushuka zaidi ya ilivyo sasa.
“Lakini
kwa sababu bei inashuka kila mara, ni lazima tukae na kuangalia mwenendo wake
ili kuamua kama tuendelee au tusiendelee na uchimbaji. Ikiwa ndani ya miaka
miwili hali itakuwa hivi katika bei, tutalazimika kuufunga mgodi ndani ya miaka
miwili kuanzia sasa,”Mutereko alisema.
Alifafanua
kuwa fedha wanazozitumia kuchimba madini ni nyingi hivyo ni afadhali wakafunga
maeneo mengine kuruhusu yaendelee yenye faida na mafanikio makubwa.
“Dhahabu
inayotoka katika mgodi huu huwezi kuilinganisha na ya North Mara, ile ni nyingi
na ni bora zaidi, hivyo bei zinapozidi kuporomoka ni afadhali unaendelezwa
zaidi ule wenye faida kubwa na kufunga mingine. Hilo tutalijua baadaye, ngoja
tutazame mabadiliko ya bei sokoni,” alisema.
Post a Comment