Miley Cyrus, Drugs zamtupa Hospital.

20140503-035848.jpg
Mwanamuziki Miley Cyrus ambae hivi karibuni alisimamisha show zake za Tour iliyokua ikiendelea kwa ajili ya utambulisho wa album yake mpya, inasadikika kuwa alitumia Drugs kupita kiasi mpaka kufikia kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospital ambapo alikaa siku kadhaa kwa ajili ya matibabu na kufanikiwa kurudi katika ulingo wa stage tena.
Kutokana na cover na story ndani ya “Life & Style Magazine”, Miley Cyrus baada ya kula ‘Bata’ kwa miezi kadhaa pamoja na pombe na ‘Bangi’ sana, alizima masaa kadhaa bila kujijua ikanidi akimbizwe hospitali kwa ajili ya matibabu na kusababisha kuahirisha baadhi ya show zake zinazoendelea sasa hivi duniani.
20140503-054429.jpg
Shahidi mmoja ambae kati ya watu waliomuona mwanadada huyo akipiga ‘Bata Refu’ alisema kuwa, June 2013 akiwa na rafiki zake katika moja ya week end za mwezi huo huko ‘Palm Springs’, aliwaona wakipiga Beer na Cocktails kwenye pool, halafu bibie akawastua waende kwa nyuma ya mjengo wakavute Bangi. Walipofika kwenye kona hiyo bibie Miley Cyrus akatoa bonge la mfuko likiwa limejaa ‘weed’ na kuendeleza Bata hilo kwankwenda mbele, Kwa mujibu wa mshirika huyo anasema bangi hiyo ilikua kali sana na mwanadada Miley alikua anapiga ‘Puff’ za hatari ambapo baadae mmoja kati ya marafiki hao alizidiwa nguvu na bata hilo akakimbizwa hospitali na kulazwa.
20140503-055604.jpg
Utumiaji huu wa vilevi tofauti unasababisha kuzungumziwa na vyombo vya habari vya nchini marekani kuwa, mashabiki wa mwanadada huyu wanaweza wakachukulia hii ni tabia isiyokubalika na kuanza kukataa kumpa support.

Post a Comment

أحدث أقدم