Warembo
wanaowania taji la Miss Dar City Center 2014 wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hii leo.
Mratibu wa shindano hilo, Judith Michael akizungumza na wanahabari, pamoja nae ni Mkufunzi wa warembo hao.
*********
Na Father Kidevu Blog
WANYANGE
20 wanao wania taji la Miss Dar City Center kesho Mei 16 mwaka huu
watawasha moto vikali katika ukumbi wa Maisha Clab wakati wa shindano
lao la Vipaji.
Shindano
hilo litaongozwa na wasanii, Rich Mavoko, Bonge la Nyau na TID ‘Mnyama’
wanataraji kuwaongoza warembo hao kuwania taji la Vipaji 'Miss Talent
Dar City Center 2014."
Akizunguumza
na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo mratibu wa Shindano hilo,
Judith Michael Amesema warembo wote 20 wapo katika hali nzuri na
wamejifua vya kutosha kwaajili ya shindano hilo la vipaji.
“Tunaamini
shindano la mwaka huu litakuwa zuri sana warembo wamejiandaa vya
kutosha, tunapenda kwaalika wadau mbalimbali wa masuala ya urembo waje
kwa wingi Club Maisha siku hiyo ya Ijumaa ili waweze kushuhudia wenyewe
jinsi warembo wa jiji letu walivyojaliwa vijapaji hakika miss Tanzania
yupo Dar City Centre,” alisema Judith.
Aidha
Judith amesema shindano la Miss Dar City Centre litafanyika Mei 24 mwaka
huu katika ukumbi wa Escape One Mikocheni ambapo pia ameahidi shindano
hilo kuwa la aina yake.
Judith
amewataja warembo wanao wania taji hilo kuwa ni pamoja na Naomy
Kisaka, Nasreen Abdul, Gladys Matson, Habiba Israel, Jenny Zahn,
Doreen Elias, Winniefrida Msusa, Grace Mella na Rehema Athumani.
Wanyange
wengine ni Francisca Simon, Salha Suleiman, Dorica Daud, Agriphina
Yelezwa, Sabina Thomas, Jihan Dimachk, Aziza Thabiti, Hatma Rshidi
Nyembo na Neema Sisamo.
Huku
wadhamini wa Shindano hilo la Miss Dar City Centre ni Prima Total Hair
Collection,Gumbo Investment Diamond Bureau Dechange, Father Kidevu Blog,
Maisha Club,Q Plus, Zanzi Cream, Clouds Fm, Machapta, Flamour
Cosmetics, Valley Spring, Best Point Hotel, Atik Aluminium, Jambo Leo,
Blog Ya Wananchi na Skylight Band.
إرسال تعليق