Je unamkumbuka mkalimani huyu
aliyeuduwaza ulimwengu kwa utafsiri wake wa ishara wakati wa mazishi ya
hayati mzee Nelson Mandela mwaka uliopita ?
Thamsanqa Jantjie aliyekashifiwa na ulimwengu
mzima na haswa walemavu kwa kutoa ishara zisizotafsirika kwa wale wenye
matatizo ya kusikia wakati wa mazishi ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini
Nelson Mandela sasa amepata ajira .Jantjie alijitetea kuwa alishikwa na kiwewe na kuona mazingaombwe wakati wa maziko hayo.
Tangazo hilo la linapigia debe mtandao wa kijamii wa Livelens uliotengezwa na kampuni moja kutoka Tel Aviv Israili.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Max Bluvbland ameiambia BBC kuwa Jantjie yuko timamu na kuwa alitekeleza majukumu yake bila tashwishi yeyote ''yeye ni mtu timamu aliyepatikana na mkasa anaojutia.
Wataalamu wa lugha za ishara walisema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu alikanusha kuwa kulikuwa na suala la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alionekana akisimama kwenye jukwaa wakati wa ibada hiyo iliyokuwa ikitizamwa kote duniani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Post a Comment