Maafisa
nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea
katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya
dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka
kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari
sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko
huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako
zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi
Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini |
Waandishi
wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya
gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu
waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo
lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza
mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini
shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda
wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.
Post a Comment