
Huku akiwa anasuburia kunyakuwa tuzo za MTV zinazotarajiwa kufanyika
tarehe 7 june, Diamond amechaguliwa kuwania tuzo za BET katika category
ya "Best International Act (Africa)
Diamond anachuwana na mwanadada Tiwa Savage (Nigeria), Davido (Nigeria),
Mafikizolo (South Africa), TOOFAN (Togo) na Sarkodie (Ghana)
Diamond anasema hakutarajia kabisa kama angechaguliwa katika tuzo hizo
kwasababu hajawahi kuwasiliana nao hata siku moja. Akiongea kutoka
London amesema wakati yuko set akiendelea na ku record video yake mpya,
manager wake Babu Tale ndio alimwambia amechaguliwa BET ila akadhani ni
utani , ila baada ya kuona tweets nyingi za mashabiki ndio akaamini.
إرسال تعليق