Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kutoka kwenye ndege ya
kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukaa
angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha.Katibu Mkuu amewasili Zanzibar kwa
ajili ya mkutano wa hadhara utakaofanika kwenye viwanja vya mikutano vya
Kibanda Maiti.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye ndege
ya kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya
kukaa angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya
hewa kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha. Katibu Wa NEC ameongozana na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mvua kubwa ikinyesha Zanzibar ambapo CCM inatazamiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Mitaa mbali mbali ikiwa imefurika maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
إرسال تعليق