MWANDISHI ATUHUMIWA HUJUMA KENYA



picha_b72ac.jpg
Serikali ya Kenya imeombwa kumkamata na kumuwasilisha haraka mwandishi habari Walter Barasa katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu iliyo mjini Hague. Mwandishi huyo anatuhumiwa kuhujumu shughuli za koti hiyo kwa kuwashawishi mashahidi kubadilisha au kutotoa ushahidi kenye kesi dhidi ya makamu wa Raisi wa Kenya William Ruto anayeshtakiwa pamoja na Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa madai ya kuhusika katika ghasia zilizozuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Mwito huu umetolewa na mshirikishi wa mahakama ya ICC nchini Kenya Bi Maria Camara alipouzuru mji wa Kisumu. chanzo: VOA

Post a Comment

Previous Post Next Post