
The Standard, hotel ambayo Jay Z na shemeji yake Solange walizipiga mbele ya Beyonce siku ya junatatu tarehe 5 May 2014 kwenye lift za hotel hiyo na kudakwa na cctv camera. Hotel hiyo imetangaza kuwa mfanyakazi huyo ambae alikuwa shift usiku huo amefukuzwa kazi katika hotel hiyo kwa kosa hilo. Bado haijaeleweka rasmi kama mfanyakazi huyo ni mwanaume au mwanamke lakini hotel imesema wameweza kumgundua aliesababishia hotel hiyo aibu kwa kuvunja sheria za hotel hiyo za kuweka privacy ya wateja wake na atashtakiwa kutokana na vifungu vya sheria.
TMZ ambao ndio walioachia video hiyo inasemekana kuwa mfanyakazi huyo alipewa kiasi cha $250,000 kwa kuweza kuwapa video hiyo ambayo imeangaliwa na watu wengi sana duniani kwa muda mfupi sana.
إرسال تعليق