Wasanii wa filamu Jacob Stephan aka JB ,King Mjuto, Vicent
Kigosi aka Ray na mwanadada Irene Uwoya wanatarajia kuondoka usiku wa
kuamkia Jumatano hii kwenda Uturuki kujifunza utamaduni za nchi hiyo
pamoja na kukutana na waigizaji wakubwa wa nchi hiyo.
Uongozi wa Princess Casino pamoja na wasanii wa filamu
Wasanii hao ambao amepata udhamini Princess International Casino
wamesema safari hiyo ya wiki moja wataitumia kwenda kujifunza mambo
mbalimbali yatayowasidia kukuza sanaa yao. Akizungumza na waandishi wa
habari akiwa Princess Casino ndani ya IT Plaza Jijini Dar es salaa,
mmoja kati ya wasanii hao,Jacob Stephan amesema kuwa wameahidiwa na
Princess International Casino kwenda kukutana na watu muhimu kwenye
tasinia yao.
“Princess Casino wametuahidi kule tutakutana na watu muhimu sana
kwenye shughuli ambayo tunafanya,kwangu mimi naiita hii ni fursa
kwasababu ni vitu ambavyo tulikuwa tunaomba,” alisema.
Pia kwa upande wake mchekeshaji mkongwe King Majuto amedai kuwa
katika safari hiyo atajifunza na kuangalia tamaduni za watu wa Uturuki.
“Mimi nimefurahi sana kwenda Uturuki,huu ni mwanzo mutasikia Majuto kahamia Uturuki, safari yangu ni kujua utamaduni wao,mimi nimefarijika sana kwenda kubadilisha mawazo kwa mapuMziko. Hii ni heshima kubwa sana kwangu haswa,kwasababu niliganda hapa mpaka nafa, leo nimepata faraja ygingine tena isije ikaniua,” alisema.
Chanzo:- bongo5

إرسال تعليق