Zilipita
headlines nyingi za Diamond kufanya kolabo na mastaa wakubwa wa muziki
Afrika akiwemo Davido na Iyanya, video zake kuchezwa kwenye tv za
kimataifa na zinazoonekana sehemu kubwa ya Afrika kama Trace TV, MTV
BASE, Channel O na Sound City, zikaja headlines kwenye tuzo kubwa za
Afrika kama MAMA Awards na sasa hii ya Brazil imefatia.
Taarifa ikufikie kwamba wimbo wa Diamond wa number 1 rmx ft. Davido
umechezwa kwenye mall inayotembelewa na mamia ya watu kila siku iitwayo
Morumbi ndani ya mji wa Sao Paulo ambao mpaka mwaka 2011 ulikua na
wakazi zaidi ya milioni 11.

Wimbo wa Diamond ulisikika kwenye spika za mall hii ambayo naambiwa ina ukubwa wa mara tatu zaidi ya Mlimani City Dar es salaam.
Ndani ya hii mall ya Morumbi naambiwa kuna studio kubwa ambayo kuna
Dj maalum ambae anapiga nyimbo mbalimbali ambazo zinasikika kwenye mall
nzima kupitia spika kwenye kona mbalimbali.

Haijajulikana ulifika vipi na Dj aliupata vipi ila tunafatilia kujua ilikuaje kupitia kwa ripota wa nguvu Mtanzania Terry Sudi
ambae ndio aliusikia na kushout kwa furaha kuona mbongo mwenzake
anapata nafasi kwenye nchi kama Brazil japo hawaelewi kinachoimbwa.

إرسال تعليق