PICHA HII HAISADIFU UHALISIA WA TUKIO
KAHAMA
MWANAFUNZI mmoja mkazi wa Jijini Mwanza Clinton Majembe ameuwawa kwa
kupigwa na mama yake wa kambo Lupinda Kauli Mwalimu wa Shule ya Msingi Malunga
mjini Kahama kwa kinachodaiwa kuwa kuwa mtoto huyo aliacha jiko jiko la gesi likiwa
linawaka ndani.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven ambapo tukio hilo lilitokea
usiku wa kuakia Ijumaa kuu alisema kuwa Marehemu alikuwa ni Mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule moja mjini Bukoba.
Mseveni
alisema kuwa Marehemu Clinton alikuja kumsalimia mama yake wakati wa likizo
ndogo ya pasaka na hivyo kumkosa hali ambayo ilisababisha mama yake huyo wa
kambo aliyekuwepo katika nyumba hiyo kupiga kutokana na kudai kuwa alikuwa
amewasha jiko la gesi bila ya idhini yake.
HAPA NIKIFANYA MAHOJIANO NA MWENYEKITI WA MTAA WA MAJENGO NOELE MSEVEN
Alisema
kuwa Mama huyoa ambaye ni mtu wa matukio katika mtaa huo pia inasadikiwa pia
aliwahi kmtishia mume wake kumuua na hivyo kusababisha kuukimbia mji wake mpaka
kufikia hivi sasa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Ernest Mangala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kudai kuwa kwa sasa hayupo ofisi yupo nje kikazi na kuhaidi kulizunguzia
tukio hilo pindi atakaporejea kazini hivi karibuni.
Picha Na:- bundalawilliam
إرسال تعليق