Nguruwe wanaorandaranda kupigwa risasi India

Wanaharakati wamepinga vikali kuwaua Nguruwe wakisena ni kinyume na haki za wanyama
Mji wa Shivpur nchini India umejikuta matatani baada ya maafisa wake kuwataka watu wanaomiliki bunduki kuwapiga risasi Nguruwe wanaozurura mjini na kuwa kero kwa wakazi.
Wakazi waliamrishwa kubeba bunduki zao pamoja na lesenei zao kuthibitishwa wana idhini ya kumiliki bunduki ili kuweza kushiriki zoezi hilo. Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Hindustan Times Newpaper
Maafisa wa utawala walisema kuwa wataweza kuwapa mikataba watu watakaoteuliwa kushiriki katika zoezi la kuwapiga risasi Nguruwe wanaorandaranda mjini humo, kulingana na malipo watakayotaka.
Waliongeza kuwa wale watakaoruhusiwa kuwaua Nguruwe hao watateuliwa mwezi Mei.
Kero la Nguruwe wanaorandaranda mitaani nchini India
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu wamekasirishwa sana na pandekezo hilo la serikali.
‘‘Huu ni unyama na sio suluhu la tatizo la wanyama hao kurandaranda mjini,’’alisema Puneet Tripathi, mwasisi wa shirika la kutetea haki za wanyama na mazingira.
‘‘Lazima maafisa wangalie njia zengine za kusuluhisha tatizo hilo labda kwa kuwahamisha wanyama hao hadi katika mji mwingine,’’ aliongeza bwana Puneet.
Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwapiga risasi Nguruwe itakuwa kinyume na sheria za India kuhusu ukatili.
Nguruwe wameonekanakama kero sio mjini humo pekee bali pia katika miji mingine nchini India. Huonekana mara kwa mara wakipekuwa kwenye majaa ya taka wakitafuta chakula.
- bbc

Post a Comment

أحدث أقدم