Ni majonzi wazazi wakiandamana Nigeria

Wazazi wa wasichana 230, waliotekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamefanya maandamano kuiomba serikali ya Nigeria kuongeza juhudi na kasi ya kuwatafuta watoto wao waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Wazazi waliandamana kuishinikiza serikali kuongeza kasi ya kuwatafuta watoto waoWasichana hao walikuwa wanafunzi katika mji wa Chibok na walitekwa nyara wakijiandaa kufanya mitihani yao zaidi ya wiki mbili zilizopita.
‘‘Tunataka kuona juhudi zaidi,’’ alisema mama huyoMzazi mmoja ambaye hakutaka kutajwa , alisema kuwa wanashukuru wanigeria kwa kuwaunga mkono huku maandamano mengine yakifanyika kuwashinikiza maafisa wakuu.
Kundi la wapiganaji la Boko Haram, halijasema chochote kuhusu madai kwamba wapiganaji wake ndio waliowateka nyara wasichana hao usiku wa tarehe 14 mwezi Aprili.
Wazazi walijawa na majonzi wakati wa maandamano wakisema serikali inajikokota
Kundi hilo ambalo linapinga elimu ya kimagharibi , limekuwa likifanya mashambulizi Kaskazini mwa Nigeria, na inakisiwa kuwa watu 1,500 wamepoteza maisha yao mikononi mwa kundi hilo mwaka huu pekee.

Mnamo siku ya Jumatano, mamia ya wanawake waliandamana wakiwa wamevalia nguo nyekundu licha ya mvua kubwa kunyesha na kutembea hadi majengo ya bunge mjini Abuja kuwasilisha ujumbe.
Wanailalamikia serikali kwa kusema haifanyi juhudi za kutosha kuwanusuru wasichana hao.
"Tunawashukuru wanawake waliotuunga mkono,'' alisema mama huyo akiongeza kuwa maandamano huenda yakashinikiza serikali kuongeza kasi ya kuwatafuta watoto wao.
Tunawaomba na wale walio huko nje kuja kutusaidia kwa sababu huu ni msiba mkubwa kwa wazazi wetu.
Alipokuwa anaongea, kilio na mayowe yaliweza kusikika kutoka kwa akina mama wengine waliokuwa wanaandamana.

Awali waziri wa mambo ya ndani wa Nigeria aliambia BBC kuwa alielewa hisia za wanawake hao, lakini serikali haiwezi kufichua inachofanya

Post a Comment

Previous Post Next Post