Toka
March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba
zaidi ya watu 200 haijulikani ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea
Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa siku zote hizo toka imepotea ndugu wa abiria wa ndege hiyo
wamekua wakishinda kwenye hoteli ambazo pia zimekua zikitumiwa na
shirika hilo la Malaysia kukusanyika na kutoa taarifa kuhusu
kinachoendelea kwenye kuitafuta ndege hiyo.
May 1 2014 taarifa zimeanza kusambaa kwamba ndugu hao sasa wamepewa
maagizo waondoke kutoka kwenye hoteli zote walizofikia Beijing na Kuala
Lumpar na kurudi nyumbani kwao ambapo taarifa za chochote kitakachotokea
watazipata wakiwa hukohuko majumbani.
Hii
iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena vilio na kupiga mayowe baada ya
kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la ndege inamaanisha haitakuwepo
tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye chumba cha mikutano kwa ndugu
hao kupewa taarifa za kinachoendelea kwenye zoezi la utafutaji wa ndege
hiyo.
Kwenye hoteli ya Lido Beijing ambako kampuni hiyo ya ndege imekua
ikiwalipia ndugu hao wa abiria toka ndege ipotee, kulikua na watu
wanaozidi 500 ambao wote ni ndugu wa abiria waliopotea.
Hata hivyo kampuni hii ya ndege itaanza kutoa malipo ya pesa kwa
ndugu hao siku za karibuni ambapo japo haijasema itatoa kiasi gani,
sheria inasema ndugu wanaweza kulipwa kuanzia dola za kimarekani laki
moja na nusu mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti mpya iliyotoka inasema maafisa hawakua wamegundua kupotea kwa
ndege hiyo mpaka dakika 17 baadae na walichelewa kwa dakika 240 kuanza
kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea kwenye radar.
Post a Comment