Uvamizi mpya ambao umefanyika jana katika mji wa ‘Gamboru Ngala’ karibu kabisa na border ya Nigeria na Cameroon ambapo askari wa kigaidi wakiwa na silaha, waliwapiga risasi wananchi waliokuwa wanajaribu kutoroka. Senator wa mji huo Sen. Ahmed Zanna amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya wananchi 300 wameuwawa na hii inatokana na askari wa Jeshi la Nigeria waliokuwa wanalinda mji huo kuondoka kwenda kusaidia utafutaji wa wasichana wa shule ambao walitekwa na Boko Haram tarehe 14 mwezi april.
Utekaji nyara huo ambao umeustua dunia mpaka sasa, Nigeria wanepewa msaada na nchi kama UNITED STATES, FRANCE, BRITAIN, FRANCE na CHINA kusaidia utafutaji wa wanafunzi hao ambao wanasadikika kuwa inawezekana kabisa kuwa wameshasambazwa na kutolea nchini humo na tayari wengi wao watakuwa wameshavuka mipaka ya nchi hiyo.
Baada ya Police Force ya nchini Nigeria kutangaza dau la kiasi cha dola za kimarekani $300,000 sawa na €215,000 baada ya Boko Haram chief ‘Abubakar Shekau’ kuachia video ya kusema kuwa atawauza wasichana hao kama watumwa na wengine wataolewa na wanajeshi wa jeshi lake. Katika utekaji nyara wa huo wa pili uliofanyika jana, Boko Haram walibeba wasichana wengine wapatao 11 ambao ni kati ya umri wa miaka 12 mpaka 15 ndani ya state ya BORNO.
US President ‘Barack Obama’ ameelezea kuwa ‘Chibok abductions’ ni “heartbreaking and outrageous”, na amesema kwamba timu ya wataalam wa kijeshi kutoka Marekani imeshaingia nchini Nigeria na tayari wameshaanza kazi ya kutafuta wanafunzi hao. British Prime Minister ‘David Cameron’ siku Jana amesema kuwa utekaji nyara huu wa watoto wa kike ni “pure evil” na ofisi yake imeshatuma wataalam wa kijeshi kusaidia upatikanaji wa wanafunzi hao kuweza kurudi nyumbani kwenye familia zao. French Foreign Minister Laurent Fabius amesema pia kuwa “special team” ipo tayari nchini Nigeria’s na kazi inaendelea kusaidia upatikanaji wa wasichana hao huku Rais wa nchi hiyo ‘Jonathan’ amesema kuwa ‘Chinese Premier Li Keqiang’ ametoa ahadi ya kutoa msaada wa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Post a Comment