Serikali ya Nigeria
inasema kuwa iko tayari kuzingatia mbinu zote zitakazowezesha kuachiliwa
huru salama kwa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule waliotekwa nyara
na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Awali waziri wa serikali alikuwa ameshikilia msimamo mkali kama vile kukatalia mbali pendekezo la kiongozi wa Boko Haram la kubadililishana wafungwa wa Boko Haram wanaozuiliwa na serikali na wasichana hao.
Wakati huohuo, jamaa namarafiki wa wasichana hao waliotekw anyara wameweza kuwatambua baadhi ya wasichana kutoka katika kanda ya video iliyotolewa na kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu siku ya Jumatatu.
Familia za wasichana hao ziliweza kutazama kanda hiyo ambapo Shekahu alisema sharti serikali iwaachilie wafungwa wao kabla ya wao kuwaachilia wasichana hao ambao kundi hilo limesema wameweza kuwasilimisha.
'Usaidizi wa kigeni'
Marekani imesema inapeleka vifaa vya uchunguzi nchini Nigeria kusaidia katika juhudi za kuwatafuta wasichana wanaozuiliwa na kundi la Boko Haram.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shule moja Kusini mwa eneo la Borno mwezi mmoja uliopita.
Msemaji wa Rais Obama Jay Carney amesema kikosi cha maafisa 30 kiko nchini Nigeria tayari kushiriki juhudi hizo.
Amesema msaada huo wa Marekani kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi na pia kutoka idara ya uchunguzi ya FBI.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati baadhi ya Jamaa za wasichana waliotekwa nyara wakielezea majonzi baada ya kutazama kanda ya video iliyotolewa na kundi hilo.
'Matumaini'
Baadhi wameiambia BBC kuwa kanda hiyo imewapa matumaini lakini wameshangaa kuona wasichana hao ambao wengi ni Wakristu wamevalia mavazi ya Kiislam.
Akizungumza kwa uchungu nduguye mmoja wa wasichana waliotekwa ameiambia BBC ni heri kanda hiyo ingeonyesha maiti za wasichana hao kwa kuwa hiyo ingeondoa wasiwasi unaoendelea kukithiri na kuumiza mioyo ya wengi.
Kwenye kanda hiyo ya video kiongozi wa Boko Haram , Abubakar Shekau anasikika akiambia serikali ya Nigeria yuko tayari kubadilishana baadhi ya wasichana hao na wafuasi wake waliofungwa jela.
Seneta Ali Ndume kutoka eneo ambapo wasichana hao walitekwa nyara anaisihi serikali kulegeza msimamo.CHANZO BBC,(A.I)
إرسال تعليق