Alisema kufuatia wizi huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu wawili kwa uchunguzi zaidi.
Ofisi za Gazeti la Daraja Letu, zilizopo eneo la
Uwanja wa Ndege mjini Njombe, zimevunjwa na kuibwa nyaraka muhimu
mbalimbali na kompyuta tano.
Akizungumzia wizi huo kwa mwandishi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Daraja, ambalo ni wachapishaji wa gazeti hilo, Simon Mkina alisema wizi
huo uliotokea usiku wa Aprili 30, mwaka huu.
Akizungumzia mazingira ya wizi huo, Mkina alisema dalili zinaonesha
kuwaulipangwa ama na baadhi ya watu wanaojua vyema taratibu za kazi za
shirikalake, au watu wenye uhusiano wa karibu na ofisi hiyo.
"Kuna uwezekano mkubwa wa kuhusika kwa watu wa karibu na shirika letu,
lakini kwa kuwa tayari Polisi imeanza kazi zake, ni vyema tukaliacha
Jeshihilo likaendelea na matokeo yake tutaambiwa," aliongeza Mkina.
Mkurugenzi huyo pia alisema huenda asili ya kazi za gazeti lao, hasa
habariza uchunguzi, ikawa sababu nyingine ya wahusika wa wizi huo wa
nyarakakuhusika.
"Siwezi kueleza moja kwa moja iwapo habari zetu za uchunguzi zikawa
chanzopia, lakini si chanzo cha kupuuza, maana utendaji wetu umekuwa
mwiba kwawatendaji wabovu wa Halmashauri," alisema Mkina.
Gazeti la Daraja Letu limekuwa likiandika habari za utendaji
usioridhishawa baadhi ya viongozi wa halmashauri za mikoa ya Njombe na
Iringa, kufuatilia matumizi ya fedha na pia kuibua changamoto za maisha
namaendeleo kwa mikoa hiyo miwili.
Post a Comment