Mwimbaji maarufu wa Pop, Miley Cyrus ambaye alilazwa
hospitalini mwezi uliopita baada ya kusumbuliwa na allergy na flu,
amewekwa chini ya uangalizi mkali wa matabibu.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, mwimbaji huyo ameruhusiwa
kuendelea na ziara yake nchini Uingereza ambayo aliisitisha kwa muda
lakini muda wote atakuwa chini ya uangalizi wa matabibu kwa kuwa afya
yake hubadilika ghafla na kuishiwa nguvu mara kwa mara.
“Miley amekuwa chini ya matabibu wawili ambao wanaangalia maendeleo
yake ya afya masaa 24 akiwa nyumbani. Tayari ameshapewa matabibu ambao
watakuwa standby muda wote wakati akiwa kwenye ziara yake ya Uingereza.
Kitu kibaya sana ni kwamba ugonjwa wake huwa unatulia kabisa na anakuwa
mzima lakini ghafla anaugua tena.” Chanzo kimeliambia gazeti la Daily
Mirror.
Imeripotiwa kuwa muda wote alipokuwa hospitalini alikuwa hawezi kula
vizuri na kwamba hadi sasa anatumia matunda na mboga za majani ili
kuongeza vitamini zaidi mwilini na haruhusiwi kuvuta kitu chochote.
“Sasa hivi anawekwa chini ya uangalizi makini wa chakula na anakula
matunda na mboga za majani ili kuongeza vitamin na amezuiwa kutumia
vinywaji vikali au kuvuti kitu chochote hususani bangi.” Kimeeleza
chanzo hicho.
Post a Comment