
Anabaki: Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United.
BEKI mfaransa, Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United , klabu imethibitisha.
BEKI mfaransa, Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United , klabu imethibitisha.
Evra alitazamiwa kuondoka baada ya United kuweka ofa ya paundi milioni 27 kwa beki wa kushoto wa Southampton , Luke Shaw.
Lakini beki huyo ameamua kubakia kwa mwaka mmoja katika ubosi wa kocha mpya Louis vanGall.
Mapema wiki hii, Evra aliripotiwa kuwa
na mazungumzo na Juventus, lakini sasa atapambana na Shaw katika namba
yake endapo tu Man United itafanikiwa kumsajili beki huyo wa kimataifa
ya Uingereza majira ya kiangazi mwaka huu.
Kitendo cha Evra kuongeza mkataba
kitapokelewa kwa furaha na mashabiki wengi wa Man United ambao wana
mapenzi ya moyoni na beki huyo mwenye miaka 33 tangu alipojiunga na timu
hiyo mwaka 2006 akitoka Monaco.
Evra pia ni mchezaji anayependwa na wenzake katika vyumba vya kubadilishia nguo, pia anasifiwa kwa uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Beki huyo wa zamani wa Nice,
aliyeichezea United mechi 379 alionesha kiwango kizuri msimu uliopita,
licha ya klabu kudoda katika kipindi hicho cha David Moyes.
Aliifungia
United bao la kuongoza katika mchezo wa robo fainali ya UEFA dhidi ya
Bayern Munich, japokuwa haikutosha kuwabakisha kwenye mashindano katika
uwanja wa Allianz Arena.

Evra (kulia) kwasasa yupo katika kambi
ya timu ya taifa ya Ufaransa kujiandaa na fainali za kombe la dunia
mwezi ujao nchini Brazil
Post a Comment