Mkuu
wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Singida, Bw.
Saidi Majimoto, akihamasisha wanafunzi wa ualimu kujinga na mfuko wa
PSPF ili kujihakikishia kupata mafao ya kukidhi mahitaji.Kushoto ni
afisa wa PSPF, Andrew Mtima.
Baadhi
ya wanafunzi wa ualimu chuo cha Lake Hill mjini Singida,wakimsikiliza
mkuu wa mfuko wa pensheni kwa watumisi wa umma (PSPF), Saidi Majimoto
(hayupo kwenye picha)akiwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili kufaidika
na mafao lukuki.
Bango la PSPF.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MFUKO
wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) unakusudia kujenga nyumba 200
za gharama nafuu mkoani Singida kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake.
Mkuu
wa PSPF mkoani Singida, Said Majimoto alieleza hayo hivi karibuni
wakati akitambulisha Mfuko huo kwa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Lake
mjini hapa.
Majimoto
amesema kuwa mfuko huo umechukua hatua hiyo ili kuwawezesha wanachama
wake kuishi mahali pazuri pasipo na usumbufu na kwa kwa bei nafuu
kabisa.
Amesema
kuwa kwa hivi sasa michoro ya viwanja hivyo, ambavyo vipo eneo la
Mandewa iko tayari na kwamba ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kuanza
wakati wowote.
Majimoto
alifafanua kuwa PSPF hutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama waliochangia
miaka mitano na kuendelea ambapo hulipa kidogo kidogo kupitia mishahara
yao kwa muda wa miaka hadi 25. “Mwanachama huanza kuishi katika nyumba
yake mara tu anapoanza makato ya mkopo husika” amesema.
Aidha,
alidokeza kuwa PSPF hutoa mikopo ya fedha kwa kiwango cha hadi nusu ya
mafao ya mwanachama aliyebakiza miaka mitano kustaafu, kwa ajili ya
ujenzi, ukarabati na ununuzi wa nyumba mahali popote anapoamua
mwanachama huyo.
Mhasibu
wa mfuko huo kutoka Makao Makuu, Andrew Msina amesema kuwa hadi sasa
mfuko huo una wanachama 400,000, kati ya idadi hiyo asilimia 97 ya
walimu walio kwenye ajira ni wanachama. Alisema kuwa wingi huo wa
wanachama unatokana na ukweli kwamba PSPF ina aina ya kikokotoo bora
zaidi kuliko mfuko mwingine wowote wa jamii nchini.
Msina
pia amesema kuwa hadi Juni 2013 PSPF ilikuwa imelipa mafao ya sh.
bilioni 543.7 kwa wastaafu mbalimbali nchini huku Mfuko huo ukiwa
unajivunia thamani ya mafao ya sh. trilioni 1.25 kibindoni.
إرسال تعليق