Rapper Quick Rocka amesema anajisikia ni mtu mwenye bahati kubwa
baada ya Nahreel kukubali kuwa producer wa studio yake, Switch Records.
Quick aka Switcher ameiambia Bongo5 kuwa Nahreel ni producer mkali
kwa sasa nchini hivyo kufanya kazi naye kutaiweka studio yake sehemu
nzuri na anajisikia furaha kufanya naye kazi. “Tunafanya kazi kwa
makubaliano tu na tunawekeana target, siwezi nikasema kama nimemwajiri
ni kama partiner wangu. Namiliki studio lakini yeye ni kama partner
wangu,” amesema Quick.
Amesema hadi sasa kupitia studio hiyo, Nahreel ameshatayarisha nyimbo kadhaa ukiwemo wimbo wa Joh Makini na wa Izzo B.
إرسال تعليق