
Ray J msanii ambae aliachia video wakifanya mapenzi na mpenzi wake wa zamani ‘Kim Kardashian’ mwaka 2004 ambayo ilisababisha gumzo kubwa sana katika vyombo ya habari duniani kote na kumfanya bibie huyo kuwa maarufu zaidi duniani.
Kim Kardashian ambae jumamosi ya tarehe 24 anafunga pingu za maisha na msanii ‘Kanye West’ amezawadiwa kiasi cha dola za kimarekani $47,000 kama zawadi ya harusi ambacho kiasi hicho cha fedha kimepatikana kwenye mauzo ya Sex Tape iliyotoka miaka hiyo wakati wapenzi hao waliifanya wakiwa wapenzi. Video hiyo ambayo imetengeneza zaidi $50 Million, Kim amekataa zawadi hiyo na Ray J ameahidi kutoa pesa hizo kwenye charity ya Kim Kardashian.
Ray J amekuwa kwenye maisha ya Kim baada ya mwanadada huyo kurudiana na msanii Kanye West na kuchukua mahusiano yao katika sura nyingine, Ray J aliachia ngoma ijulikanayo kama “I Hit it First” na kufanya video ambayo alimuweka msichana ambae anafanana kabisa na mwanadada Kim, na nyimbo hiyo ikiwa na maneno kama yeye msanii Ray J ndio alikuwa wa kwanza kwa mwanadada huyo. Kwa mtazamo wa watu wengi sana ni kwamba msanii Ray J kama ana panic hivi sababu maneno yake yote hayo lakini mwanadada huyo hajawahi kumjibu.
Post a Comment