MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana alifunga bao tamu sana na kuinusuru Real Madrid kupoteza mechi.
Valencia
ilionekana kubeba pointi zote tatu Uwanja wa Santiago Bernabeu, lakini
mshindi huyo wa Ballon d'Or aliinusuru timu yake tena, alipounganisha
krosi ya Angel di Maria kwa utaalamu wa hali ya juu.
Mathieu
alianza kuifungia Valencia dakika ya 44, lakini Sergio Ramos
akaisawazishia Real Madrid dakika ya 59na Parejo akawafungia wageni bao
la pili, kabla ya Ronaldo kufunga lake la 50 msimu huu.
Licha ya
Atletico kufungwa 2-0 na Levante jana, bado ipo kileleni mwa La Liga kwa
pointi zake 88 za mechi 36, ikifuatiwa na Barcelona pointi 85 mechi 36
wakati Real sasa ni ya tatu kwa pointi zake 83 za mechi 35.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bonge la bao jana katika sare ya 2-2 na Valencia
Ronaldo (katikati) akimtoka mchezaji wa Valencia, Juan Bernat (kushoto)
إرسال تعليق