Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni
vya ovyo–havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya,
nilitazama kipindi cha ‘BIBI BOMBA’ kinachorushwa na TV hiyo.
Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa
hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.
Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa ‘Biology’,
akajibu ‘ndiyo’. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale
ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale
walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali
kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.
Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali
hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV!
Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale
kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile
siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone
kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu
wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya
maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo
halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo
watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia.
Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi
wanaoshiriki
إرسال تعليق