
Waziri
wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema
‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari
wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara
za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni
kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha
Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia
yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake
treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa
‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo
vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni
lazima uwepo kwa saa 24′

Kazi
hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es
salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa
tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha
Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi
ya watu elfu moja.
إرسال تعليق