Simba yamzuia straika ligi kuu kusaini mkataba

 
STRAIKA wa Tanzania Prisons, Six Ally Mwakasega, ambaye ni mmoja wa nyota wanaotakiwa na Klabu ya Simba, amesema yupo tayari kujiunga na vijana hao wa Msimbazi iwapo tu watampa maslahi mazuri.
Six alijiunga na Prisons msimu uliopita akitokea Majimaji ya Songea ambayo ipo Ligi Daraja la Kwanza.
Akizungumza na Championi Jumatano, Six ambaye amemaliza mkataba na kikosi cha Prisons, alisema amesitisha zoezi la kusaini mkataba mpya na kikosi hicho kwa kuwa anataka kusikiliza ofa nyingine, ikiwemo ya Simba.
Alisema kuhusiana na Simba amekuwa akisikia tetesi za kutakiwa na klabu hiyo na yupo tayari kujiunga nayo iwapo tu watampa maslahi mazuri, kwani mpira ni kazi yake.
“Niliitwa na kiongozi wa Prisons kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya lakini sitasaini, nazisikiliza kwanza ofa nyingine. Kuhusu Simba nimekuwa nikisikia inanitaka lakini binafsi hawajanifuata,” alisema Six ambaye ni mmoja wa wachezaji muhimu wa kikosi hicho.

Post a Comment

أحدث أقدم