Stamina afunguka na kuelezea ukimya wake pamoja na ushindi wa Fid Q KTMA

stamina

Stamina
Rapper kutoka Morogoro, Stamina amefunguka kuhusu ukimya wake pamoja na ushindi wa Fid Q kwenye KTMA 2014.

Stamina amedai alikuwa kimya kutokana na masomo
na kufanya mambo yake mengine ya kumwingizia pesa.
“Ukiachana na muziki mimi ni mwanafunzi wa chuo,kuna muda nafanya muziki na kuna muda nayapa masoma nafasi,” amesema. “Kwahiyo ukiona hivyo nipo kimya kwenye muziki nilikuwa nafanya shule. Katika maisha kila mtu anapata riziki kivyake hata huyo shabiki haingizi hela kwa kusikiliza nyimbo zangu,na yeye ana kazi zake nyingine anafanya,kila mtu ana jinsi ya kuingiza hela. Tatizo la muziki wa bongo naujua bila kitu mbadala, yaani sidhani kama unaweza ukafanya vitu vya maana. Sasa mimi ni mwanafunzi na kuchanganya shule na muziki inakuwa vigumu,usipokipa kila kitu muda wake unaweza ukafeli. Kwahiyo ukiona nipo sana kimya ujue muda huo nipo shule nasoma lakini nikipata nafasi natoa ngoma. Hata hivyo sio muda mrefu sana kuna kolabo ya Songa, kuna kolabo ya Joh Maker zote zipo redioni, bado zinasikika redioni,kwahiyo hizo kolabo pia zimenifanya niache kwanza kutoa ngoma yangu. Sasa hivi nakuja full, kuna kolabo ya mimi na Nay wa Mitego,kuna kolabo ya mimi na Stereo na mimi nina ngoma zangu tatu ambazo sijajua nitoe ipi? Ila Jumatatu nitatoa jibu ninatoa ipi.”
Pia Stamina amedai kuwa ushindi wa Fid Q kwenye tuzo za Kili ni sawa na baba yake kushinda bingo ya milioni 100 kwahiyo mtoto atakuwa na furaha.
“Ushindi ya Fid Q ni sawasawa na baba yako kashinda bingo ya milioni 100 ,mtoto lazima ufurahi” amesima. ” Kwahiyo ushindi wa Fid Q ni ushindi wa Hip Hop. Kama mimi ni shabiki wa Fid lazima nifurahie hicho kitu,nilikuwanae kwenye category moja lakini mimi nilikuwa najichukulia poa sana. Nilikuwa napenda sana Fid achukue tuzo, miaka mingi sana wanamzingua. Kwahiyo walivyofanya ni vizuri sana na Kili sasa hivi kidogo wameona aibu sana kumnyima tuzo Fid Q, kwahiyo kumpa Fid tuzo ni kiroho safi yaani,nimefurahi sana hata yeye anajua.”
-  Credit:- Bongo5

Post a Comment

Previous Post Next Post