Stamina |
Rapper kutoka Morogoro, Stamina amefunguka kuhusu ukimya wake pamoja na ushindi wa Fid Q kwenye KTMA 2014.
Stamina amedai alikuwa kimya kutokana na masomo
na kufanya mambo yake mengine ya kumwingizia pesa.
“Ukiachana na muziki mimi ni mwanafunzi wa chuo,kuna muda nafanya
muziki na kuna muda nayapa masoma nafasi,” amesema. “Kwahiyo
ukiona hivyo nipo kimya kwenye muziki nilikuwa nafanya shule. Katika
maisha kila mtu anapata riziki kivyake hata huyo shabiki haingizi hela
kwa kusikiliza nyimbo zangu,na yeye ana kazi zake nyingine anafanya,kila
mtu ana jinsi ya kuingiza hela. Tatizo la muziki wa bongo naujua bila
kitu mbadala, yaani sidhani kama unaweza ukafanya vitu vya maana. Sasa
mimi ni mwanafunzi na kuchanganya shule na muziki inakuwa
vigumu,usipokipa kila kitu muda wake unaweza ukafeli. Kwahiyo ukiona
nipo sana kimya ujue muda huo nipo shule nasoma lakini nikipata nafasi
natoa ngoma. Hata hivyo sio muda mrefu sana kuna kolabo ya Songa, kuna
kolabo ya Joh Maker zote zipo redioni, bado zinasikika redioni,kwahiyo
hizo kolabo pia zimenifanya niache kwanza kutoa ngoma yangu. Sasa hivi
nakuja full, kuna kolabo ya mimi na Nay wa Mitego,kuna kolabo ya mimi na
Stereo na mimi nina ngoma zangu tatu ambazo sijajua nitoe ipi? Ila
Jumatatu nitatoa jibu ninatoa ipi.”
Pia Stamina amedai kuwa ushindi wa Fid Q kwenye tuzo za Kili ni
sawa na baba yake kushinda bingo ya milioni 100 kwahiyo mtoto atakuwa na
furaha.
“Ushindi ya Fid Q ni sawasawa na baba yako kashinda bingo ya milioni
100 ,mtoto lazima ufurahi” amesima. ” Kwahiyo ushindi wa Fid Q ni
ushindi wa Hip Hop. Kama mimi ni shabiki wa Fid lazima nifurahie hicho
kitu,nilikuwanae kwenye category moja lakini mimi nilikuwa najichukulia
poa sana. Nilikuwa napenda sana Fid achukue tuzo, miaka mingi sana
wanamzingua. Kwahiyo walivyofanya ni vizuri sana na Kili sasa hivi
kidogo wameona aibu sana kumnyima tuzo Fid Q, kwahiyo kumpa Fid tuzo ni
kiroho safi yaani,nimefurahi sana hata yeye anajua.”
إرسال تعليق