MSHAMBULIAJI
Luis Suarez ameongeza tuzo katika orodha yake ya tuzo, baada ya kutajwa
ndiye Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya England 2013/14.
Nyota
huyo wa Liverpool amefunga mabao 31 na kutoa pasi 12 za mabao katika
mechi 33 za Ligi Kuu alizocheza, huku timu yake Liverpool ikizidiwa kets
kidogo na Manchester City katika mbio za ubingwa.
Suarez,
ambaye pia ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa PFA na
Mchezaji Bora wa Waandishi wa habari za Soka msimu huu, alinyakua tuzo
ya nne msimu huh baada ya Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England.
Anahitaji kabati kubwa la mataji: Luis Suarez akionyesha tuzo sake mvili binafsi za Ligi Kuu England
Na hii
pia: Awali Suarez akiwa na mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi
wa Mwaka, Eden Hazard alishinda tuzo za PFA mwezi uliopita
Mpachika
mabao huyo wa Uruguay, ambaye anajiandaa kukutana na England katika
Fainali za Kombe la Dunia Juni 19, alimaliza msimu akiwa mfungaji bora-
akimzidi kwa mabao 10 mchezaji mwenzake wa Wekundu hao, Daniel
Sturridge.
إرسال تعليق