“Tangu
kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni
kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya
sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu
Uongozi
wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry ya Sumbawanga, Rukwa umetoa ubani wa Sh5.5
milioni kwa familia za ndugu na jamaa waliofariki dunia kutokana na
ajali ya moja ya mabasi yake iliyotokea Aprili 28 katika Kijiji cha
Utaho, Wilaya ya Ikungi, Singida.
Katika
ajali hiyo, watu 19 wakiwamo polisi wanne, walifariki papohapo baada ya
kugongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali
hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori na mwendesha
baiskeli ambaye alipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kugongwa na
lori hilo. Wakazi hao waliogongwa walikuwa wamekusanyika kushuhudia
ajali hiyo.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipoliti Daniel Kholani alisema rambirambi
hiyo ilikabidhiwa kwa Serikali ya Kijiji na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone ambaye naye alichangia Sh100,000.
Kholani
alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa
Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia
wamechanga Sh600,000.
“Tangu
kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni
kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya
sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.”
Kholani
alisema wakazi wa kijiji hicho, Mussa Mohammed, Suku Abdallah na Ayubu
Ramadhani bado wamelazwa hospitalini wakiendelea kutibiwa majeraha
waliyoyapata kwenye ajali ya basi hilo ambalo bado lipo Kituo cha Polisi
Ikungi.Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry ya Sumbawanga, Rukwa
umetoa ubani wa Sh5.5 milioni kwa familia za ndugu na jamaa waliofariki
dunia kutokana na ajali ya moja ya mabasi yake iliyotokea Aprili 28
katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi, Singida.
Katika
ajali hiyo, watu 19 wakiwamo polisi wanne, walifariki papohapo baada ya
kugongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali
hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori na mwendesha
baiskeli ambaye alipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kugongwa na
lori hilo. Wakazi hao waliogongwa walikuwa wamekusanyika kushuhudia
ajali hiyo.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipoliti Daniel Kholani alisema rambirambi
hiyo ilikabidhiwa kwa Serikali ya Kijiji na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone ambaye naye alichangia Sh100,000.
Kholani
alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa
Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia
wamechanga Sh600,000.
“Tangu
kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni
kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya
sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.”
Kholani
alisema wakazi wa kijiji hicho, Mussa Mohammed, Suku Abdallah na Ayubu
Ramadhani bado wamelazwa hospitalini wakiendelea kutibiwa majeraha
waliyoyapata kwenye ajali ya basi hilo ambalo bado lipo Kituo cha Polisi
Ikungi.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment