Quick Rocka adai anajisikia mwenye bahati baada ya Nahreel kukubali kuwa producer wa studio yake .

Quick Rocka

Rapper Quick Rocka amesema anajisikia ni mtu mwenye bahati kubwa baada ya Nahreel kukubali kuwa producer wa studio yake, Switch Records.
Quick aka Switcher ameiambia Bongo5 kuwa Nahreel ni producer mkali kwa sasa nchini hivyo kufanya kazi naye kutaiweka studio yake sehemu nzuri na anajisikia furaha kufanya naye kazi. “Tunafanya kazi kwa makubaliano tu na tunawekeana target, siwezi nikasema kama nimemwajiri ni kama partiner wangu. Namiliki studio lakini yeye ni kama partner wangu,” amesema Quick.
Amesema hadi sasa kupitia studio hiyo, Nahreel ameshatayarisha nyimbo kadhaa ukiwemo wimbo wa Joh Makini na wa Izzo B.

Post a Comment

Previous Post Next Post