Stori: Na Gabriel Ng'osha
OFISA Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface
Wambura akizungumzia kuhusiana na mapato yaliyotokana na mechi kati ya
Taifa Stars na Zimbabwe iliyochezwa wiki iliyopita ambapo jumla ya
shilingi milioni 63 zilipatikana baada ya mashabiki elfu kumi na moja
kujitokeza kuangalia mchezo huo.
Pia alizungumzia kuhusu siku ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
ambayo itaanza kuchezwa Agosti 24 mwaka huu ambapo ligi hiyo itahusisha
timu 14 na tiketi za eletroniki zitatumika .
Pia kurudi kambini kwa timu ya Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa
marudiano dhidi ya timu ya Zimbabwe mchezo utaopigwa Juni mosi mwaka
huu jijini Harare, Zimbabwe. Pia TFF wameandaa safari ya mashabiki
watakaohitaji kwenda na timu nchini humo kwa kuchangia gharama ya
shilingi laki tatu kwenda na kurudi.
إرسال تعليق