
Meneja
Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamthilia ya redio iitwayo
‘Kinga ya Moyo Wangu’ itakayoelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa bima
jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mkazi wa Kampuni ya BIMA
inayotoa huduma za bima kupitia simu za mkononi, Christian
Karlander. Tamthilia hiyo itasikika katika vipindi vya Jahazi na Leo
Tena vya Clouds FM.

Meneja
Mkazi wa Kampuni inayotoa huduma za bima kupitia simu za mkononi ya
bima Tanzania, Christian Karlander (kulia) akionyesha kipeperushi wakati
wa uzinduzi wa tamthilia ya redio iitwayo ‘Kinga ya Moyo Wangu’
itakayoelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa bima jijini Dar es Salaam
jana. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.

Meneja
Usambazaji wa Kampuni inayotoa huduma za bima kupitia simu za
mkononi ya bima Tanzania, Donald Galinoma (kushoto) akizungumza wakati
wa uzinduzi wa tamthilia ya redio iitwayo ‘Kinga ya Moyo Wangu’
itakayoelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa bima jijini Dar es Salaam
jana. katikati ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, leo imezindua tamthilia ya ‘Kinga
ya Moyo Wangu’ itayokuwa inarushwa hewani kila siku kwa wiki nane na
kituo cha utangazaji cha Clouds FM ambacho kitatoa elimu na kuhamasisha
watumiaji wa simu za mkononi wa mtandao wa tigo kujiunga na bidhaa ya
pona na Tigo bima.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez amesema tamthilia hiyo maridhawa yenye
matukio ya kusisimua itawavutia wasikilizaji pamoja na kuwaelimisha
watanzania kuhusu manufaa ya bima.
“Kampuni
ya simu za mkononi kama Tigo ina wajibu katika kuwapatia wateja wake
huduma na bidhaa zenye gharama nafuu. Sambamba na jinsi teknolojia
ilivyoweza kuleta mageuzi katika namna ambavyo tunaweza kutuma na
kupokea fedha barani Afrika,”
“hivi
sasa tupo tayari kufanya hivyo kupitia bima ya simu. Tigo inayofuragha
kuwa mstari wa mbele katika hatua hii kubwa kwa ajili ya Tanzania,
ukuaji wa uchumi wake na maendeleo ya taifa nzima,” amesema Gutierrez.
Amesema
kwamba programu hiyo ya redio imefadhiliwa na benki ya maendeleo ya
Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuelimisha umma umuhimu na faida ya kuwa na
bima wakati wote.
Kwa
upande wake , Meneja Mkazi wa Bima Tanzania, Christian Karlander
amesema kuwa tamthilia hiyo itarushwa mara mbili kwa siku kwa muda wa
wiki nane kupitia vipindi vya Jahazi na Leo Tena.
“Mradi
huu umezinduliwa na Bima, Kampuni inayoongoza kwa kutoa bima kupitia
teknolojia ya simu za mkononi nchini Tanzania, ambayo inatoa huduma ya
bima ya maisha nay a kulazwa hospitalini jijini Dar es Salaam kupitia
mtandao wa simu wa Tigo,” amesema
Karlander
aliongeza kuwa takribani milioni 4.6 ambayo ni asilimia 19 ya watu
wazima nchini wamewekewa bima, lakini ni kupitia bima za waajiri wao au
chini ya mikopo hata hivyo, kiwango cha watanzania waliojiandikisha bima
kwa hiari ni ndogo sana.
“Jijini
Dar es Salaam, Bima imesajili zaidi ya wateja 500,000 baada ya miaka
miwili tu ya kuanza kufanya kazi nchini, na asilimia 79 ya wateja hao ni
watu wenye vipato chini ya dola 2.50 (shilingi 4,215) kwa siku,”
aliongeza Karlander
Alisisitiza
kuwa bidhaa hiyo ya bima kuanzia gharama ya shilingi 750 na kiwango cha
juu ni shilingi za kitanzania 4,000 kwa mwezi na Bima inalipa mpaka
shilingi 600,000 pindi mteja anapolazwa hospitalini au kufariki dunia.
إرسال تعليق